MAFANIKIO NI KATIKA MUDA
Habari za leo rafiki yangu?
Karibu sana kwanye makala ya leo ambayo ni yapekee kwenye mafanikio katika maisha yako juu ya namna ya kutumia muda ili kuleta mafanikio makubwa katika malengo unayoyaweka kila siku katika maisha yako.
Karibu sana kwanye makala ya leo ambayo ni yapekee kwenye mafanikio katika maisha yako juu ya namna ya kutumia muda ili kuleta mafanikio makubwa katika malengo unayoyaweka kila siku katika maisha yako.
Mafanikio katika maisha maana yake ni utumiaji mzuri wa muda katika mambo yanayoleta maendeleo chanya katika maisha yako, pia kushindwa kufanikiwa maana yake ni utumiaji usio sahihi wa muda katika mambo yasioleta maendeleo katika maisha yako ya kila siku.
Ukifuatilia kwa umakini juu ya historia za maisha ya watu waliofanikiwa duniani kote utagundua ya kuwa ni watu wenye kujali kila sekunde, dakika, lisaa, masaa (muda kwa ujumla) katika maisha yao, ndiomana wakawa wamefikia kwenye kilele cha mafanikio makubwa kwa haraka kila wanapoweka malengo yao. Kwa hiyo kwa ujumla ni watu wenye kujali muda wakijua yakuwa mafanikio yao yako katika utumiaji mzuri wa muda wao.
Watu wengi hii leo wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kila wanapoyaweka si kwasababu hawawezi kuyafikia lahasha bali ni kwasababu ya kushindwa kutumia muda kwa usahihi kwenye mambo yanayoweza kuleta mabadiliko katika maisha yao bali wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mambo yasioleta hata robo ya badiliko katika maisha yao na wakibaki kulalamika kuwa maisha ni magumu pasipokujua tatizo ni namna bora ya utumiaji sahihi wa muda katika mambo yenye kuleta maendeleo na mafanikio katika maisha yao kwani muda haurudi nyuma katika maisha ya mafanikio hata siku moja.
Je wataka kujua kuwa huwa hufikii malengo yako kwa kuwa hutumii kwa usahihi muda wako? Wawezajiuliza siku ya leo tangu ulipoianza ni mambo gani ulioyapanga kuwa utayafanya na hukuyafanya? Na je sababu za kutoyafanya ni kweli zinaonyesha uzito wa kushindwa kuyafanya ukiangalia? Je katika ratiba yako ya leo kwenyemambo unayohitaji kuyafanya je mambo hayo ulioyapanga yanachangia asilimia ngapi ya kufikia malengo ulioyaweka juu ya mafanikio katika maisha yako? Je ni jambo gani ambalo si lalazima kulifanya ukalifanya likavuruga ratiba ya malengo ulioyaweka siku ya leo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo waweza jiuliza na kujua kuwa kila unachokifanya kinaangalia namna unavyotumia muda.
Rafiki muda ndio sehemu ya mafanikio yako pasipo kujua namna nzuri ya kutumia muda utajikuta unalalamika kuwa kwanini hufanikiwi na kuanza kumtafuta mchawi wa mafanikio yako pasipokujua kuwa mchawi ni wewe mwenyewe . Yawezekana hujajua sasa ufanye nini ili uwezetumia muda wako vizuri hebu jifunze mambo yafuatayo ili uweze jua namna ya kutumia mda wako kwa mafanikio mazuri.
Weka malengo yenye kuleta maendeleo katika maisha yako.
Siku zote watu wenye kuweka malengo yenye maendeleo katika maisha yao ni wale ambao wanapoamka asubuhi wala hawakimbilii sim zao na kuanza kujibu sms za kwenye magrup ya watsap na facebook ambazo ziliingia wakiwa wamelala wala si watu wa kuamka na kuanza kusikiliza nyimbo mpya za bongofleva au kuangalia move wazipendazo kwakuwa wanajua muda ni wathaman sana kwao bali ni watu ambao wanapoamka wanafikiria ni malengo gani wanapaswa kuyafanyia kazi siku hio nzima wanahakikisha wamebanwa na ratiba zao kiasi ya kwamba hawana muda wa kupoteza katika jambo lolote lisilo na msingi katika siku hio. Rafiki usikubali SIM , TV au kitu chochote kikachukua mudawako hebu panga nini unahitaji kufanya siku ya leo ambacho kina mchango mkubwa katika kuleta mafanikio yako alafu uanze nacho bila kuchelewa kabisa. Na utakapo anza kukifanya usikubali kushindwa hakikisha unakamilisha kwa muda uloweka.
Sema hapana.
Watu wengi wanashindwa kusema hapana ratiba zao zinapoingiliwa na mambo ambayo si muhimu na kujikuta wanashindwa kukamilisha walioyapanga mfano ni muda wa kazi mtu anachati na kujibu sms kwa muda ambao sio wa kuchati lazima ufeli tu. Siku zote huwezi fanya mambo yalio kwenye ratiba na yasio kwenye ratiba lazima utafeli tu kwakuwa muda ni mchache wa kukamilisha mambo ulioyapanga na bado ukaongeza mengine yasiokuwa kwenye ratiba na kujikuta siku inaisha pasipo kufanya jambo lolote la maana.Rafiki hebu usikubali jaambo lolote lisilo kwenye ratiba kuingilia ratiba yako kama ratiba inasema ni mda wa kuchati chati kama ni muda wa kusoma soma usichanganye mambo kwani muda hausubiri na ukipoteza sekunde moja umepoteza kitu kikubwa katika maisha.
Fanya kwa umakini na kwa mda kitu ulichopanga kukifanya.
Hebu hakikisha kitu ulichopanga kukifanya kwa wakati huo unakifanya tena kwa muda uliojiwekea usikubali kufanya huku unafanya vitu vingine mfano unafanyakazi kidogo alafu unaingia watsap kidogo lazima utavuruga tu unachofanya, lazima ubongowako uuambie sasa ni muda wa kazi au muda wa kusoma au ni muda wa kufanya kitu hiki ili kusudi kwamba ukifanye kwa umakini ubongo ukiwa uko huru ndipo utakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kuwa makini na unachofanya na hatimae kupata mafanikio ya hali ya juu. Hebu siku ya leo jaribu kufanya kitu bila ya kuchanganya na vitu vingine visivyo na maana utaona mafanikio yasio ya kawaida.
Rafiki napenda kukushauri kuwa kila unalotaka ufanikiwe jua kutumia muda wako nawe utafanikiwa bila
shaka.
Hebu rafiki mshirikishe na mwingine ujumbe huu ili ajue kuwa muda niwathaman sana kwake kwake
kuliko anavyofikiri.
Emmanuel Daud.
Sim: 0679329339
Email: daude950@gmail.com
Post a Comment