MAMBO MAWILI (2) HATARI KATIKA MAISHA YA MAFANIKIO
Habari rafiki karibu tena katika makala ya leo ambayo ni yakuvutia
na ya pekee katika maisha yako karibu sana.
Rafiki katika maisha waweza kukubaliana na mimi kuwa kuna vitu
hatari ambavyo jamii au hata wazazi wetu hutukataza kuwa tusivifanye kwakuwa ni
hatari katika maisha mfano wizi ni kitu ambacho wazazi, walezi na jamii kwa
ujumla hutuambia kuwa ni hatari katika maisha.
Lakini pia katika engo au eneo la mafanikio katika maisha pia kuna
vitu ambavyo ni hatari na watu wengi wamekuwa wakivikumbatia pasipo kujua kuwa
ndo chanzo cha maisha yao kutokuwa vizuri na kuto kuwa na uwezo wa kuona mbali
kimalengo na kimawazo maishani mwao, hebu rafiki karibu usome vitu hivyo
ambavyo ni hatari na yawezekana na wewe ndivyo ulivyo vikumbatia mpaka sasa
pasipo kujua kuwa ndio chanzo cha maisha yako kuwa hivyo yalivyo sasa.
Mambo hayo hatari ni haya yafuatayo;
1. kukubaliana na maisha ulionayo bila kutafuta suluhisho la kujitoa
kwenye maisha hayo ulionayo.
Rafiki yawezekana ulemavu ulionao ndio unaokufanya ukubaliane na
maisha ulionayo maisha ambayo si maisha mazuri maisha yenye
kudharauliwa maisha yenye
kunyanyaswa na kutengwa na jamii au yawezekana ni umaskini ulionao katika
familia yenu ndio unaokufanya ukate tama kiasi hiko na kuamua kuridhia maisha
ulio nayo na kuishi bila kufikiria kuwa nini ufanye ili kujikomboa kutoka
katika maisha hayo au yawezekana una elim ambayo unahisi ni ndogo ambayo si
kama ya mtu flani hivi unaeishi nae jirani ambae yawezekana yeye ana DIPLOMA,
PHD, MASTERS na nk, au yawezekana ni kwasababu wewe ni mtoto yatima huna wazazi
ambao ulikuwa unawategemea sana kwa kila jambo katika maisha yako ni kweli inauma kuwakosa wazazi katika maisha
yawezekana ndomana unaamua kukubaliana na hali mbaya ya umaskini ulionayo, au
yawezekana ni ugonjwa ulionao ambao yawezekana umeambiwa na madaktari kuwa
huwezi kupona tena, ndomana umeamua kukata tama na kuamua bora liende kwa
maisha ulionayo ulio nayo, yawezekana ni mambo mbalimbali ambayo unayafikiria
akilini mwako mda huu unaposoma makala
hii.
Rafiki nikweli mambo hayo unayokumbana nayo yanauma sana nikweli
yanauma, lakini rafiki katika maisha kuna changamoto nyingi kama hizo ulizo
nazo lakini napenda nikwambie kuwa
changamoto na shida ulizonazo wapaswa uzishinde sikuzote usikubali zikushinde
hio ndio kanunini ya mashujaa
waliofanikiwa, unapaswa utumie changamoto ulizo nazo kama FURSA na
njia ya kukufanya ufikie mafanikio makubwa na yenye kukupatiya furaha, ulemavu,
umaskini, kuwa na elim ndogo, au kutokuwa na elim kabisa, uyatima, ugonjwa na
vingine vingi vinavyokukumba usikubali kamwe vikufanye ukubaliane na maisha
mabaya ulionayo sasa bali kwa hivyo hivyo ulivyo unaweza kuupindua ulimwengu
juu chini kwa mawazo, akili na ujuzi mkubwa Mungu aliouweka ndani ya ubongo
wako na kufanya maisha mabaya ulionayo yawe maisha mazuri ya kutamaniwa na kila
mtu maishani.
Rafiki sasa ni muda wa kutumia hali ulio nayo, shida ulizo nazo,
changamoto ulizo nazo kama fursa si kama changamoto tena katika maisha yako ili
kupata mafanikio, kamwe usikubali kukubaliana na maisha hayo ulio nayo na
kuamua kubweteka bila kutafuta suluhu au njia ya kupata maisha bora.
2. kuto kujiamini na kujikubali jinsi ulivyo.
Maisha yenye mafanikio yana uhusiano mkubwa na jinsi unavyo jiamini
na kujikubali, watu wengi
wamekuwa wanashindwa kufanikiwa au kufikia malengo yao si kwasababu
hawana uwezo huo
wanao lakini ni kwasababu tu hawajiamini wala kujikubali.
Kuto kujiamini huweza kukufanya usiwe na uwezo mkubwa wa kufikiri
mbali, pia hukufanya kila unalolifanya ujione kuwa unakosea na kibaya zaidi
hali ya hofu hujengeka ndani ya ubongo wako na kupelekea kila unachotaka
kukifanya punde tu unapokifikiria kwenye ubongo wako unajikuta unajikosoa
mwenyewe kuwa huwezi kufanya kitu unachokiwaza kukifanya si kweli kuwa hukiwezi
unakiweza ila ulishajijengea kuto kujiamini.
Pia hali ya kuto kujikubali jinsi ulivyo ni hatari kwako hupoteza
uwezo wa wewe kufanya lolote mbele ya watu, watu wengi wanajidharau na
kujitenga katika jamii kisa ni walemavu, au kisa wao ni maskini, au kisa wao ni
kabila flani ambalo wanahisi ni kabila linalodharauliwa sana na watu.
Rafiki muda wa kujidharau na kuto kujikubali ulivyo sio huu huu
nimuda wa kujiamini na kujikubali ulivyo watu waliowengi ambao nimatajiri
duniani ukiangalia historia zao ni watu waliokuwa na ulemavu kama ulionao,
walikuwa maskini kama wewe, walikuwa wanadharauliwa kama wewe na vingine vingi
ambavyo sijavitaja lakini siri kubwa ya kufanikiwa kwao ni kuwa ingawa walikuwa
na kasoro zote hizo hawakujidharau walijiamini na kujikubali jinsi walivyo
ndiomana hii leo tunawasoma na kuwafaham kuwa ni watu mashuhuri duniani hata
wewe unaweza kuwa kama wao chukua hatua leo jiamini, jikubali ulivyo
utafanikiwa usiwaze kuwa jamii inakusemaje bali waza kuwa ufanye nini ili jamii
ikutolee mfano kwa kila waliongealo kutokana na mafanikio ulio nayo na jinsi
unavyojikubali na kujiamini ingawa una kasoro.
Juwa kuwa shida, umaskini au kasoro uliyonayo ni FURSA kamwe
usiiangalie wala kuitumia kama shida au kasoro iangalie kama fursa maishani
mwako.
Nashukuru rafiki kwa kusoma makala hii natumaini imebadilisha maisha
yako na kuleta mafanikio makubwa yenye furaha maishani mwako.
Naomba pia umshirikishe mwenzako ujumbe huu ili uweze kumsaidia
katika maisha yake ya mafanikio.
Nakutakia mafanikio mema rafiki.
Emmanuel Daud
Waweza kutoa maoni au ushauri kupitia;
Sim: 0679329339 | 0743782086
Email: daude950@gmail.com
Post a Comment