UFUNGUO WA MAFANIKIO NI KUWA NA MAONO (VISION).
Habari rafiki natumai umzima wa afya kabisa.
Karibu tena katika blog hii ya ONA MBALI blog ambayo kusudi lake kubwa ni kukufanya utoke katika hali ya maisha ulio nayo na kuinuka zaidi kuelekea kileleni ambapo kuna mafanikio makubwa zaidi ambayo bila shaka unahitaji uyafikie.
katika makala ya siku ya leo tunakwenda kujifunza umuhimu wa kuwa na maono (vision) katika maisha hasa maisha ya mtu anaehitaji kufanikiwa na kufikia njozi zake alizojiwekea karibu tujifunze zaidi umuhimu huo wa maono.
Maono yana nafasi kubwa katika kufikia mafanikio tunayo yawaza kilasiku kwa maana nyingine maono ni barabara inayotuonyesha wapi tuelekee ni ramani, ni ufunguo wa milango ya mafanikio. Kwahio unapaswa uwe na maono kuwa baada ya miaka miwili unataka uwe wapi au baada ya mda flani unataka unataka umiliki nini, au unataka umiliki makampuni mangapi au unataka uwe wapi kimaendeleo hayo ni maono.
Pia unapaswa uwe na maono makubwa ambayo ni zaidi hata ya uwezo wako na akili zako kwani kadri unavyoweka maono makubwa ndivyo utakavyotumia nguvu nyingi na akili nyingi kuhakikisha unayafikia na hatimaye ukayafikia kweli maono hayo yenye ubora na mvuto kwa wengine hata usipoyafikia utakuwa umepata uelewa na ujuzi ambao hukuwa nao mwanzo kwahio utakuwa umepiga hatua kubwa kuelekea mafanikio, lakini ukiwa na maono madogo utabweteka na kutumia nguvu kidogo katika kuyafikia na hata ukiyafikia hayatakuwa yenye ubora na mvuto katika maisha yako.

Rafiki napenda nikwambie kuwa kuishi bila maono ni sawasawa na kuishi pasipokuwa na faida yoyote katika duni, mtu mwenye maono katika maisha yake haishi tu ilimradi anaishi anaishi kwa maono na malengo.
Hebu jiulize kama hujawahi kujiuliza kuwa wewe ni nani? kwanini unaishi? umetoka wapi? unakwenda wapi? kufanya nini? na kwanini? ukijiuliza maswali hayo na kuyafanyia kazi hutaishi tu ilimradi unaishi bali utaishi kwa malengo na kwa maono na hatimaye kufikia mafanikio makubwa na hatimae kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii.
Mwisho napenda nikushukuru kwa kujifunza nami katika makala hii ya leo. Mshirikishe na mwingine makala hii ili nae aweze kujifunza umuhim wa kuwa na maono katika maisha yake.
Ahsante sana na nakutakia maisha bora na yenye maono makubwa na mafanikio.
Sim: 0679329339
Email: daude950@gmail.com.

Post a Comment