MAISHA YA MAFANIKIO NI KAMA UKUAJI WA KIUMBE HAI

Image may contain: text
Habari rafikiyangu naamini umzima wa afya karibu tena katika blog hii ya Ona Mbali ili tuweze kujifunza mengi yatakayo badilisha maisha yako. siku ya leo tutajifunza kuwa "MAISHA YA MAFANIKIO NI KAMA UKUAJI WA KIUMBA HAI"
Katika maisha ya mafanikio huwa kuna mzunguko mkubwa hadi kufikia mafanikio watu wengi wamekuwa wakikata tamaa mapema kwa mzunguko huo kuwa mrefu na wenye kukatisha tamaa kwa mtu asie na uvumilivu.
Rafiki maisha ni kama mzunguko wa ukuaji wa kiumbe hai yako taratibu lakini yanakuwa kwa uhakika kwahio unapaswa kuyavumilia na kuto kukata tamaa kwakuwa kukata tamaa ni kama kuzidi kujisukumiza kwenye moto pasipo kujua kuwa unajisukumiza motoni.
Maisha yana mizunguko kama nane ili kufikia mafanikio yako mizunguko hio ni hii ifuatayo rafiki;
1. Fikiri.
katika maisha kufikiria ndio chachu ya wewe kukufanya ujue kuwa ni nini ufanye ili kujikwamua kutoka katika hali ya maisha ulio nayo, pia si kwamba fikra zote ziko sahihi bali fikra sahihi sikuzote ni zile zenye kukutoa mahali ulipo na kukupeleka mahali pengine ambapo hukuwahi kupafikia yaani fikra chanya au fikra angavu.
2. Wazo.
Pia katika maisha yako una wazo gani juu ya kujitoa kutoka kwenye maisha magumu ulionayo? je kama wazo unalo unafanya nini ili kufikia wazo hilo? rafiki katika maisha usiishi bila kuwa na wazo hakikisha kila siku inapoanza una wazo juu ya kujiinua kutoka katika maisha ulionayo.
3. Jaribu.
Katika maisha watu wengi wamekuwa wanaogopa kujaribu vitu katika maisha yao kisa tu waliwahi kufanya kitu siku flani wakashindwa, wengine wanaogopa kujaribu kwakuwa wanahisi watachekwa pasipo kujua kuwa kuchekwa kwao ndio mafanikio yao na pasipo kujua kuwa wanaowacheka ndio watakaokuja kuomba msaada kwao siku watakapo fanikiwa.Rafiki kunamsemo wa kiswahili unaosema kuwa "uoga wako ndo umaskini wako" acha kuogopa jaribu kufanya utaona mafaniki.
4.Fanya.
Baada ya kujaribu kitu flani kwa muda mrefu sasa unafika wakati hutakiwi kujaribu tena unapaswa kufanya kwakuwa muda wa kujaribu umeisha sasa ni muda ambao unapaswa kufanya kwa kujiamini kwakuwa kama ni majaribio ulishayafanya sana kamwe maishani usiogope kufanya kitu kwakuwa unapofanya wengine huwa hawajui unacho kifanya bali wanasikiliza na kukuangalia ufanye ili wajifunze kutoka kwako,hebu anza kufanya leo usiogope.
5.Fanya tena.
Ukisha fanya mara ya kwanza unapaswa kufanya tena ili kurekebisha makosa pale ulipo kosea kufanya kwa mara ya kwanza, rafiki usiogope kufanya kitu maranyingi maishani.
6.Tena fanya.
Sikuzote kufanya fanya kitu mara nyingi hukufanya uwe mzoefu na hiko kitu kwahio wewe endelea kufanya tu usichoke.
7. Endelea kufanya.
Huwa watu wengi wakifikia hatua hii ya kufanya tena na tena huamua kukata tamaa pasipokujua baada ya kuendelea kuwa wavumilivu ndipo wanafikia hatua ifuatayo.
8.Mafanikio hatimae.
Hii ndio sehemu ambayo wewe rafiki yangu huwa unahitaji kufika kilasiku lakini yawezekana unashindwa na kukata tamaa usiogope wala usikate tamaa unao uwezo wa kufika hapa kabisa kwa jinsi ulivyo hivyo hivyo wala usijidharau wala usiogope kisa una kasoro flani wala usiogope kisa uko yatima wala usiogope kwakuwa huna elim kamwe usihofie chochote maishani mwako kwakuwa wewe una uwezo ambao hakuna mwenye uwezo kama wako katika dunia nzima ni kwavile hujaamua kuutumia tu uwezo huo.
Anza leo kujitathimini na uanze kufanya mambo ya pekee na makubwa unaweza rafiki.
Baada ya kusoma makala hii hebu usiwe mchoyo bofya like yako ili kuona kuwa tuko pamoja pia share kwa wenzako ujumbe huu ili kuwapa hamasa kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa na kufika wanapopataka.
Emmanuel Daud
email: daude950@gmail.com
Phone; 0743782086
            0679329339

No comments