EPUKA MAWAZO NA HISIA ZENYE MTAZAMO WA KUSHINDWA.

Habari yako rafikiyangu naamini umzima na unaendelea na shughuli zenye kujenga maendeleo katika maisha yako hongera sana endelea kujibidiisha kwani mafanikio yako yapo karibu sana kuliko unavyodhani hivyo usikate tama mapema endelea kupambana.

                                
Leo napenda nikushirikishe makala hii ya leo yenye kichwa kisemacho “EPUKA MAWAZO NA HISIA ZENYE MTAZAMO WA KUSHINDWA” naamini utajifunza vitu ambavyo yawezekana hukuwa unavijua kuhusu hisia na mawazo namna vinavyochangia kufanikiwa kwako au kuto kufanikiwa kwako.


Rafiki hisia na mawazo vina mchango mkubwa sana katika maisha ya mafanikio yako, kwani ndivyo vinavyokufanya utende kitu chema au kibaya mara baada ya kukifikiria, hivyo ili kufanikiwa  katika maisha kuna umuhimu mkubwa wa kufikiria au kujihisia mawazo mazuri yenye hamasa ya kuleta ushindi/mafanikio katika maisha yako.

Hebu soma kisa hiki uone namna mawazo na hisia chanya zinavyoweza kuleta mafanikio/ushindi katika maisha;

Kulikuwa na vijana wawili ambao ni Inawezekana na rafiki yake aitwae Samwel marafiki hawa walijuana toka wapo wadogo sana,  kijana aitwaye Inawezekana yeye aliamini kilakitu kinawezekana katika maisha kama jina lake lilivyo, lakini Samweli  alikuwa ni mtu wakushindwa tuu hata katika michezo na mambo mengine, Inawezekana alikuwa akipambana hadi dakika ya mwisho katika kila jambo maishani mwake.

 Sikumoja walialikwa katika mashindano pale mtaani kwao shindano hilo lilikuwa linahusina na michezo yakuingia ndani ya gunia na kisha kukimbia ndani ya gunia hilo hadi shambani, Wengi walivyosikia hivyo walijitokeza maana zawadi ilikuwa ni kuku, basi zoezi lilianza na baada ya dakika kumi (10) watu watano walishindwa wakatolewa nje ya uwanja wakabaki watu watano ambao kati yao walikuwa ni Inawezekana na Samweli,  kila mtu katika mchezo huo aliamini kuwa hawezi kushinda kutokana na kuchoka sana katika mchezo huo, ila Inawezekana aliamini ushindi kuwa bado upo hivyo aliendelea kupambana ili kuhakikisha ushindi ni wake.

Basi vijana hawa wakaendelea kushindana lakini walikuwa wamechoka sana kiasimkwamba wakawa wanasimama na kupumzika kwa mda mrefu uwanjani hapo, hivyo kutokana na kuchoka kwao huko mkuu wa masindano  hayo aliamua kuwasimamisha na kuwauliza “Nani kati yenu anaamini kabisa atashinda katika mashindano haya?’’ Basi wote walinyamaza kimya ila Inawezekana alisema kwa hisia kali kuwa yeye anaamini kuwa atafika hadi mwisho na kushinda mashindano hayo ingawa amechoka sana, basi kauli ya ushujaa alioitoa kijana Inawezekana ilitosha kumfanya aonekane mshindi katika mashindano hayo, hivyo mkuu wa mashindano akaamua kuwa Inawezekana apewe ushindi huo kutokana na kuwa na imani kuwa hatakama amechoka kiasi gani anauwezo wa kushinda hivyo Inawezekana alipewa zawadi ile ya kuku pamoja na medali.

Rafiki naamini umejifunza namna hisia na mawazo chanya yanavyoweza kumfanya mtu kufikia anachokihitaji hata kama yuko katika wakati mgumu kiasi gani. Hivyo hata wewe nakusihi yakuwa katika maisha yako usihisi wala usiwe na mawazo ya kushindwa hatakama mazingira unayokutana nayo ni magumu kiasi gani wewe endelea kujipa moyo kuwa utashinda hata kama itatokea marafiki zako wengine watakukatisha tamaa na kukwambia kuwa huwezi ukafika unapohitaji kufika wewe usiwasikilize endelea kujitamkia kuwa unaweza .

pia katika maisha yako kama una marafiki ambao mawazo yao na hisia zao zinawaza kushindwa tu nakusihi kuwa marafikia hao kuwa mbali nao kabisa kwana watavuruga ndoto za maisha yako kabisa kabisa, tafuta marafiki ambao watakutia moyo na kukupa hamasa katika jambo ambalo unahitaji kulifanya.

Mwisho kabisa napenda nikushukuru rafikiyangu kwa kutumia muda wako katika kusoma makala hii naamini umejifunza vitu ambavyo najua vitabadilisha maisha yako.

Pia napenda kukukaribisha katika ukurasa wangu wa “ONA MBALI” ulioko  facebook kama hujajiunga utafute ukurasa huo na kisa bonyeza “like” kisha “follow” nawe utakuwa umejiunga na ukurasa huo.

Kwa ushauri au maoni  yoyote wasiliana nami;
      Sim : 0743782086
               0679329339
     Email : daude950@gmail.com
                 emarove@outlook.com



1 comment: