EPUKA MAWAZO NA HISIA ZENYE MTAZAMO WA KUSHINDWA.
Habari yako rafikiyangu naamini
umzima na unaendelea na shughuli zenye kujenga maendeleo katika maisha yako
hongera sana endelea kujibidiisha kwani mafanikio yako yapo karibu sana kuliko
unavyodhani hivyo usikate tama mapema endelea kupambana.
Leo napenda nikushirikishe makala
hii ya leo yenye kichwa kisemacho “EPUKA MAWAZO NA HISIA ZENYE MTAZAMO WA
KUSHINDWA” naamini utajifunza vitu ambavyo yawezekana hukuwa unavijua kuhusu
hisia na mawazo namna vinavyochangia kufanikiwa kwako au kuto kufanikiwa kwako.
Rafiki hisia na mawazo vina
mchango mkubwa sana katika maisha ya mafanikio yako, kwani ndivyo
vinavyokufanya utende kitu chema au kibaya mara baada ya kukifikiria, hivyo ili
kufanikiwa katika maisha kuna umuhimu
mkubwa wa kufikiria au kujihisia mawazo mazuri yenye hamasa ya kuleta
ushindi/mafanikio katika maisha yako.
Hebu soma kisa hiki uone namna
mawazo na hisia chanya zinavyoweza kuleta mafanikio/ushindi katika maisha;
Kulikuwa na vijana wawili ambao
ni Inawezekana na rafiki yake aitwae Samwel marafiki hawa walijuana toka wapo
wadogo sana, kijana aitwaye Inawezekana
yeye aliamini kilakitu kinawezekana katika maisha kama jina lake lilivyo,
lakini Samweli alikuwa ni mtu
wakushindwa tuu hata katika michezo na mambo mengine, Inawezekana alikuwa
akipambana hadi dakika ya mwisho katika kila jambo maishani mwake.
Sikumoja walialikwa katika mashindano pale
mtaani kwao shindano hilo lilikuwa linahusina na michezo yakuingia ndani ya
gunia na kisha kukimbia ndani ya gunia hilo hadi shambani, Wengi walivyosikia
hivyo walijitokeza maana zawadi ilikuwa ni kuku, basi zoezi lilianza na baada
ya dakika kumi (10) watu watano walishindwa wakatolewa nje ya uwanja wakabaki
watu watano ambao kati yao walikuwa ni Inawezekana na Samweli, kila mtu katika mchezo huo aliamini kuwa
hawezi kushinda kutokana na kuchoka sana katika mchezo huo, ila Inawezekana
aliamini ushindi kuwa bado upo hivyo aliendelea kupambana ili kuhakikisha
ushindi ni wake.
Basi vijana hawa wakaendelea
kushindana lakini walikuwa wamechoka sana kiasimkwamba wakawa wanasimama na
kupumzika kwa mda mrefu uwanjani hapo, hivyo kutokana na kuchoka kwao huko mkuu
wa masindano hayo aliamua kuwasimamisha
na kuwauliza “Nani kati yenu anaamini kabisa atashinda katika mashindano haya?’’
Basi wote walinyamaza kimya ila Inawezekana alisema kwa hisia kali kuwa yeye
anaamini kuwa atafika hadi mwisho na kushinda mashindano hayo ingawa amechoka
sana, basi kauli ya ushujaa alioitoa kijana Inawezekana ilitosha kumfanya
aonekane mshindi katika mashindano hayo, hivyo mkuu wa mashindano akaamua kuwa
Inawezekana apewe ushindi huo kutokana na kuwa na imani kuwa hatakama amechoka
kiasi gani anauwezo wa kushinda hivyo Inawezekana alipewa zawadi ile ya kuku
pamoja na medali.
Rafiki naamini umejifunza namna
hisia na mawazo chanya yanavyoweza kumfanya mtu kufikia anachokihitaji hata
kama yuko katika wakati mgumu kiasi gani. Hivyo hata wewe nakusihi yakuwa
katika maisha yako usihisi wala usiwe na mawazo ya kushindwa hatakama mazingira
unayokutana nayo ni magumu kiasi gani wewe endelea kujipa moyo kuwa utashinda
hata kama itatokea marafiki zako wengine watakukatisha tamaa na kukwambia kuwa
huwezi ukafika unapohitaji kufika wewe usiwasikilize endelea kujitamkia kuwa
unaweza .
pia katika maisha yako kama una
marafiki ambao mawazo yao na hisia zao zinawaza kushindwa tu nakusihi kuwa
marafikia hao kuwa mbali nao kabisa kwana watavuruga ndoto za maisha yako
kabisa kabisa, tafuta marafiki ambao watakutia moyo na kukupa hamasa katika
jambo ambalo unahitaji kulifanya.
Mwisho kabisa napenda nikushukuru
rafikiyangu kwa kutumia muda wako katika kusoma makala hii naamini umejifunza
vitu ambavyo najua vitabadilisha maisha yako.
Pia napenda kukukaribisha katika
ukurasa wangu wa “ONA MBALI” ulioko
facebook kama hujajiunga utafute ukurasa huo na kisa bonyeza “like” kisha
“follow” nawe utakuwa umejiunga na ukurasa huo.
Kwa ushauri au maoni yoyote wasiliana nami;
Sim : 0743782086
0679329339
Email : daude950@gmail.com
Nice jumbe
ReplyDelete