KAMWE USIRUHUSU VIKWAZO KUHARIBU MALENGO YAKO NA RAMANI YA UNAKOELEKEA

Habari rafiki, karibu katika ujumbe wa leo kupitia Blog hii uipendayo ya "ONA MBALI" Blog hii yenye kukupa hamasa katika maisha yako na kukufanya utoke katika hatua moja ya maendeleo na kwenda hatua nyingine kubwa zaidi ya kimaendeleo.
Leo napenda nikushirikishe habari ya vikwazo katika maisha na namna ya kufanya ili visikuangushe bali vikufanye uwe imara kadri unavyokutana navyo katika maisha yako.
                                            
Kuna msemo unaosema hivi;

"kadri unavyokutana na vikwazo vingi katika maisha ndio unazidi kuwa imara zaidi katika maisha"

Msemo huo una maana ya kuwa unahitaji vikwazo vingi ili uzidi kuwa imara kwakuwa pasipo vikwazo usingeliweza hata kujua fursa na kazi mbalimbali unazo zijua sasa.
Mfano kikwazo chepesi katika maisha ambacho naamini waweza kukielewa ni kuchapwa fimbo unapofeli masomo darasani kama ikatokea siku ya kwanza ukachapwa kwa sababu ya kufeli mtihani basi siku inayofuata katika mtihani utajitahidi ili usichapwe. Kwahio vikwazo ni kama kichocheo (kwa wanachemistry huita catalyst) cha kukufanya uzidi kuyatafuta mafanikio kwa nguvu zako zote.
Lakini yawezekana kwako ni kinyume na maneno ninayo yasema yawezeka vikwazo kwako vimekufanya upoteze fraha maishani mwako au yawezekana vikwazo vimekufanya ukate tamaa ya maisha kabisa hata unajihisi huna thamani tena au yawezekana changamoto na vikwazo unavyokutana navyo vimekufanya hata uikimbie familia yako kwakuwa unahisi huna uwezo tena wa kuihudumia au labda vikwazo vimekufanya uache hata kazi ambayo ilikuwa nzuri kwako au yawezekana kutokana na vikwazo umekuwa na mawazo mengi yanayokufanya ukose raha na hata kupelekea kuumwa maishani mwako au yawezekana vikwazo vimekufanya uwe hivyo ulivyo sasa.
Rafiki napenda nikwambie kuwa suluhu ya vikwazo unavyokumbana navyo maishani si kukimbia familia wala si kukata tamaa, wala si kuamua kuacha kazi, wala si kuruhusu kuwa na mawazo kiasi hicho ulicho nacho wala si kubaki kuwa mpweke kama ulivyo sasa bali suluhu yake ni kusimama imara na kuangalia malengo yalio katika ramani yako ya mafanikio ambayo umejiwekea kuwa unahitaji uyafikie.
Jua kuwa unavyo tafuta mafanikio uko katika uwanja wa vita kama komando na vikwazo ndio maadui zako wapaswa uvishinde sio vikushinde.

Mwisho kabisa nakuomba rafiki usiruhusu vikwazo kuvuruga malengo yako na ramani ya unakoelekea wewe cha msingi angalia malengo yako usiangalie vikwazo vinavyokuzunguka nawe utafanikiwa.
Napenda nikushukuru kwa kutumia mda wako kusoma ujumbe huu katika Blog hii ya ONA MBALI Blog bora kwaajili ya mafanikio ya maisha yako.
Usisahau kushea ujumbe huu kwa marafiki zako ili nao wajifunze kitu kupitia ujumbe huu wa leo.
Pia waweza kujiunga na ukurasa wangu ulioko facebook kama hujajiunga andika "ONA MBALI" kisha like ukurasa huo utakuwa umejiunga nawe utapata jumbe na makala mbalimbali nitakazokuwa nikituma kila wakati.
Kwa ushauri, maoni au shukrani waweza wasiliana nami kupitia;
           emmarove@outlook.com
Sim: 0679329339
        0743782086
Emmanuel Daud

BLOGGER WAKO APENDAE UFANIKIWE





No comments