JITAHIDI KUYAISHI MALENGO YAKO USIYASHI MALENGO YA WENZAKO.

Habari rafiki naamini umzima wa afya, karibu katika makala ya leo tena katika Blog hii ya ONA – MBALI.

Leo napenda tujifunze jambo kubwa linalowafanya wengi washindwe kufikia njozi na malengo yao, jambo lenyewe si jingine ni “KUYAISHI MALENGO YA WENGINE BADALA YA KUYAISHI MALENGO YAKO”

Rafiki katika maisha watu wengi huweka malengo tena makubwa na yenye kuvutia kiasi kwamba mtu akikuhadisia waweza kujihisi kuwa wewe huna malengo makubwa kama alionayo mtu huyo, lakini chakushangaza kadri siku zinavyokwenda ukimfwatilia mtu huyo ili kujua kuwa amefikia wapi katika yale malengo aliyokuhadisia waweza kumkuta yuko vile vile na hata chakushangaza zaidi waweza kumkuta mtu huyo anazidi kuwa na maisha magumu na mabaya zaidi ya mwanzo.

Je waweza kujiuliza ni kwanini bado yuko katika hali aliyonayo?  Je waweza kujiuliza ni kwanini  hapigi hatua kutoka pale alipo? Utakapo muuliza aweza kuwa na majibu mengi yenye kuonyesha namna alivyokata tama, pia aweza kukueleza majibu mengi yenye kuilalamikia familia, serikali, jamii, marafiki na majibu mengi sana kama hayo lakini mbali na hayo ukweli ni kwamba mtu huyo “ANAYAISHI MALENGO AMBAYO SIO YAKE”  yani ni mtu anapenda kufanya kila jambo analoliona likifanywa na watu wengine.

Katika maisha unapoweka lengo kuwa utanunua shamba ekari tano kwaajili ya kulima nyanya au mahindi  au umeweka lengo kuwa utafungua genge ili uuze vitu mbali mbali kama vile nyanya, vitunguu na n.k lakini baada ya muda kwasababu umemuona jirani yako amefungua kibanda cha chipsi na wewe ukaamua kuyaishi malengo ya jirani yako hivyo ukaamua na wewe kufungua kibanda cha chipsi kwakuwa tu unahisi kama jirani yako anapata faida sana kwahiyo ukaamua kuachana na malengo yako ulioyaweka ya kufungua genge au kununua ekari tano kwaajili ya kulima nyanya au mahindi.

Rafiki kuyaishi malengo ya wengine katika maisha ni utumwa mkubwa sana unaopelekea watu wengi kubaki katika hali  ya umaskini maisha yao yote, hivyo nakushauri rafikiyangu kuwa jikubali kubali malengo uliojiwekea na chukua hatua kuyatimiza kwani malengo yako uliojiwekea yako bora kuliko unavyofikiri, usishawishiwe na mtu awaye yote kujaribu kubadili malengo  yako kwa kumuiga hata kama iweje chamsingi fanya kile unachokiamini kuwa kina faida kwako na kile ambacho nisehemu ya malengo yako uliojiwekea.

Mwisho kabisa napenda nikwambie kuwa katika maisha kutokana na bidii yako, mafanikio yako, utofauti wako, mawazo yako, “WAFANYE WENGINE WAYAISHI MALENGO YAKO SIO WEWE KUYAIHI MALENGO YAO”

kwa makala nyingine zaidi karibu katika ukurasa wangu ulioko facebook unaotambulika kwa jina la “ONA – MBALI” utafute kisha like na follow ukurasa huo nawe utakuwa umejiunga na ukurasa huo.
Kwa ushauri, maoni, mapengekezo wasiliana nami kwa;

            emmarove@outlook.com

Sim: 0743782086
         0679329339

EMMANUEL DAUD BLOGGER WAKO APENDAE UFANIKIWE


No comments