WAWEZA FIKIA MALENGO YAKO KWANI WEWE NI WAPEKEE



Habari yako rafiki na heri ya mwaka mpya mwaka 2017.

Napenda kukukaribisha sana katika blog hii ambayo kusudi lake ni kukupa hamasa juu ya mafanikio katika maisha tulionayo hapa katika ulimwengu huu.

Changamoto zimekuwa nyingi kwenye maisha  hata kusababisha watu wengi kutofikia malengo ambayo wamejiwekea kwa mda mwingi.Tumaini lipo rafiki kuwa waweza fikia malengo yako kiurahisi hata kama changamoto ni nyingi kiasi gani kama tu utaruhusu mawazo chanya kufanya kazi katika ubongo wako na kuona mbali kama tai na kugundua kuwa mbele ya changamoto ulizo nazo ndipo mafanikio yako yallipo.


Huwa kwenye maisha kila kinachomtokea mtu humtokea kwa sababu na mtu asipofikiria kwa makini kuwa changamoto anayokumbana nayo imetokea kwa sababu huweza kujikuta anakuwa mnyonge, mtu mwenye huzuni na kulia kila wakati anapofikiria changamoto alizo nazo  pia anaweza kujiona kuwa ni mtu asie faa katika jamii pia mwingine hufikia hatua ya kutokujiamini kuwa ana uwezo  wa  kufanya kitu flani na kufanikiwa vizuri zaidi kwasababu tu kila alipokuwa akijaribu kufanya kitu flani na kushindwa kufanikiwa mara kadhaa  akaamua kukata tama na kujiona kuwa hawezi tena kufanya kitu na akafanikiwa katika maisha na hii ni hatua ambayo si nzuri katika maisha ya mafanikio.

Hivi wajua kuwa hakuna mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri  kwa namna ya hali ya juu, kubadili maisha ulio nayo na kuweka malengo makubwa naya hali ya juu na kuyafikia kama wewe,je wajua hilo?  Waweza kusema hapana kwa haraka punde tu uliposoma hapo juu kuwa una uwezo mkubwa,je wajua kwanini umesema huna uwezo huo punde uliposoma hapo juu?

Nikwasababu ya kuto kujiamini, kuto kujaribu,kuto kujikubali jinsi ulivyo, lakini napenda nikwambie kuwa unao uwezo hujafaham tu kuwa unao uwezo. Kwenye maisha mawazo hasi yanayoonyesha nia ya kushindwa ni hatari sana kwenye mafanikio wapaswa usikubaliane nayo hata kidogo ondoa dhana ya kushindwa weka nia ya kuwa unaweza jaribu mara nyingi kufanya kitu hata ukishindwa mara kadhaa jaribu kwani kuna msemo unaosema ”practice makes parfect kadri unavyofanya kitu unajijengea uwezo wa kukiweza.

Jua katika maisha hakuna alieubwa akawa anajua moja kwa moja  kuweka malengo na kuyafikia bali watu wanajifunza kutokana na kukosea kwao na pia wanajifunza kutoka kwa wengine namna wanavyofanya vizuri na kufanikiwa.chamsingi jikubali jinsi ulivyo, usikubali kukatishwa tama na mtu yeyote,jifunze kutoka kwa wengine, toa mawazo ya kushindwa kwenye akili yako kwakuwa wewe si wakushindwa.

Mpendwa mwisho kabisa jua kuwa wewe ni wapekee kuliko mtu awae yote na pia una uwezo mkubwa kuliko mtu awae  yote na unaweza kuwa mfano mzuri na mtu wa kuigwa katika jamii kwa mafanikio ambayo utayapata kutokana na juhudi zako ambazo ni tofauti na za mtu yoyote. Nakutakia mafanikio mema.

Mpendwa naomba umshirikishe mtu mwingine ujumbe huu ili uwe hamasa na msaada katika maisha yake.

Emmanuel Daud
Simu: 0679329339
Email: daude950@gmail.com


No comments