UNAHITAJI MAAMUZI MAGUMU ILI KUFIKIA MALENGO YAKO



Habariyako rafikiyangu pole na hongera kwa mapambano makali unayoendelea nayo naamini unaendelea kupiga hatua kuelekea mafanikio hongera sana.

Leo napenda nikushirikishe jambo ambalo naamini kama utalifanyia kazi utafika mbali sana katika maisha yako jambo ambalo linawashinda wengi katika maisha jambo lenyewe si linguine ni juu ya “KUWA NA MAAMUZI MAGUMU KATIKA MAISHA” Unaweza kujiuliza kuwa hivi kweli maamuzi yana uhusiano wowote na mafanikio? Jibu ni “NDIO” yana mahusiano makubwa sana kuliko unavyofikiri, kwani maamuzi ndio yanayomfanya mtu afikie hitimisho flani ambalo laweza kuwa zuri au baya.


Lakini maamuzi haya yanaweza kuwa na hitimisho baya pale mtu anapohitimisha maamuzi hayo  vibaya, mfano mtu ambae kakutana na maisha magumu na akaamua kujinyonga kutokana na ugumu wa maisha hayo  mtu huyu ameamua kuchukua maamuzi mabaya ambayo suluhisho lake si kujinyonga bali lilikuwa ni kupambana na maisha hayo mpaka kuhakikisha anafanikiwa.

Hata wewe unapaswakuwa na maamuzi magumu lakini yenye matokeo chanya katika maisha yako ili kuhakikisha unafikia malengo yako bila kuangalia wengine watakuonaje au watakuchukuliaje juu ya maamuzi unayotaka kuyachukua chamsingi maamuzi hayo baada ya kuyafanya yawe na matokeo chanya.

Kwahio ili ufanikiwe unahitaji kuwa na maamuzi magumu ambayo muda mwingine unaweza kujikuta hakuna anaekuunga mkono juu ya maamuzi hayo au unaweza kujikuta unasemwa sana na watu juu ya maamuzi hayo wewe usitikiswe na maneno ya watu simamia hicho ulichokiamua ilimradi tu kiwe na matokeo chanya ambayo yatakuja kuwa ni mafundisho tosha  kwa wale waliokuona kuwa umekosea kufanya maamuzi kwa wakati ule.

Unaweza kujiuliza kuwa ni maamuzi gani magumu ambayo napaswa kuyachukua ili nifanikiwe? Ni haya hapa maamuzi magumu ambayo unapaswa uyachukue ili ufanikiwe ;

1.                                            1. Kuachana na marafiki wasio na mchango wowote katika maisha yako.

Ili ufanikiwe unahitaji kuzungukwa na marafiki ambao mawazo yao yanawaza kufanikiwa tu, ukijikuta una marafiki wengi ambao wanawaza kula, kulala, kuamka, kucheza magem, kucheza michezo ya betting, kuchati whatsap, facebook,au marafiki wanaowaza wasichana kila wakati, maafiki wanaotukana matusi tukia wakati  jua kwamba hata wewe utakuwa kama wao na ukweli ni kwamba kamwe hutoweza kufikia malengo yako hata sikumoja.
Jambo la msingi ili wewe kufikia katika malengo yako chukua uamuzi mgumu wa kuvunja urafiki na watu kama hao kwani ukiendelea kuwa nao wanakuandaa kuwa tajiri wa umasikini milele katiaka maisha yako. Najia ni ngumu kuachana na watu uliowazoea lakini hunabudi kuachana nao ili kufikia njozi zako. Na utakapoachana nao tarajia kuchukiwa, kusemwa, kutukanwa na kufanyiwa mambo mengi ila hayo yasikukatishe tamaa wewe ziba masikio na fumba macho yako lenga (focus) kwenye malengo uliojiwekea uatafanikiwa.

2.                                     2. Kuachana na vitu unavyopenda kuvifanya sana na vinavyotumia muda bila faida.

Nimuhimu kuchukua maamuzi magumu juu ya vitu uvipendavyo kuvifanya lakini visivyokuletea faida katiaka maisha yako, najua nivigumu kuachana na vitu hivyo lakini jua kwamba ndivyo vinavyokufanya usiwe na maisha mazuri ambayo unayahitaji hivyo ili uwe na maisha mazuri maisha ambayo unajua yatakuawa na fraha unapaswa kuachana navyo.

vitu hivyo ni kama vile utumiaji wa mitandao ya kijamii katika shughuli ambazo hazina faida mfano mtu anakaa asubuhi mpaka jioni yuko online whatsap, facebook, twitter, instagram anachati tu au anakazi ya kupost picha kialsiku na kutafuata like nyingi napenda nikwambie kuwa huo muda unaoutumia katika shughuli hizo za kuchati ni mwingi sana na kama ungelibuni kitu chakufanya ungelifika mbali sana.

Kumbuka kuwa walioanzisha mitandao hio wao wanaingiza kipato kikubwa sana hivyo nakusihi rafiki achana na kupoteza muda kuchati katikamitandao ya kijamii bila faida bali tumia mitandao hio katika kujifunza vitu kutangaza biashara zako na kufanya mambo mengine ambayo yatakuletea faida katika maishha yako na si vinginevyo hapo ndipo utafanikiwa, najua ni vigumu kwakuwa ushaathiriwa na mitandao hio lakini unapaswa uchuke uamuzi mgumu ili kuokoa maisha yako kwani uko hatarini.

3.                                     3 . Heshimu ratiba yako.

Ili ufanikiwe unahitaji kuheshimu ratiba uliojiwekea lasivyo utajikuta unapoteza muelekeo wa unakoelekea. Unapaswa usimamie ratiba yako wakati wote na usikubali mtu akavuruga ratiba hio kwan atakuwa ameharibu uelekeo wako wote.

Wapo watu ambao wanaweka ratiba zao lakini wanakuja kuvurugiwa ratiba zao kwasababu tu hawana maamuzi juu ya kile walichojiwekea, utakuta mtu labda saa mbili ni mda wakusoma anajikuta anashawishiwa na rafikiyake kwenda kutembea nae anaenda bila kutambua kuwa anavuruga ratiba yake.

Rafiki bora watu wakuone unaringa kuliko kuharibu ratiba yako ili kuwafurahisha nafsi zao kwa vitu visivyokuwa katika ratiba yako kwa siku hio, kama mtu akija anahitaji mkatembee au anahitaji mpige stori na ukiangalia ni muda wako wakusoma mwambie haiwezekani kwakuwa muda huu ni muda wa kusoma usimfiche unapaswa umwambie hata kama atakuona unaringa ni sawa lakini atakuwa amejifunza kitu kutoka kwako kuwa muda flani unafanya kitu flani na muda flani unafanya kituflani kwahio si rahisi mtu kukuhamisha katika malengo yako chamsingi kuwa na maamuzi magumu juu ya ratiba yako usiwe kama bendera inayofwata  upepo.

Mwisho mapenda nikwambie kuwa” UNAHITAJI MAAMUZI MAGUMU ILI KUFIKIA MALENGO YAKO”

Ahsante kwa kutumia mudawako katika kusoma makala hii siku ya leo naamini umejifunza vitu siku ya leo hivyo kwakuwa wewe umejifunza vitu usisahau kushea ujumbe huu ili na wengine wapate kujifunza ulichojifunza wewe.

Pia napenda kukualika kuwa kama hujajiunga na ukurasa wangu wa “ONA MBALI” ulioko facebook muda ndo huu jiunge sasa kwani katika ukurasa huu utajifunza mengi sana ambayo naamini yatabadili maisha yako.

 Ili kujiunga na ukurasa huu uliopo facebook sachi neno “ONA MBALI” kisha bonyeza neno “FOLLOW” alafu pia bonyeza neno “ LIKE”  nawe utakuwa umejiunga na ukurasa huu wa “ONA MBALI”  

Pia karibu katika blog yangu kupitia  www.onambali.blogspot.com kwa makala nyingi zaidi.

Ila kwa ushauri zaidi au maoni yoyote waweza wasiliana nami kupitia;


Sim: 0679329339

EMMANUEL DAUD

BLOGGER WAKO APENDAE UFANIKIWE








                                                                                                                                



2 comments: