UNAHITAJI MAAMUZI MAGUMU ILI KUFIKIA MALENGO YAKO
Habariyako
rafikiyangu pole na hongera kwa mapambano makali unayoendelea nayo naamini
unaendelea kupiga hatua kuelekea mafanikio hongera sana.
Leo napenda
nikushirikishe jambo ambalo naamini kama utalifanyia kazi utafika mbali sana
katika maisha yako jambo ambalo linawashinda wengi katika maisha jambo lenyewe
si linguine ni juu ya “KUWA NA MAAMUZI MAGUMU KATIKA MAISHA” Unaweza kujiuliza kuwa hivi kweli maamuzi yana uhusiano wowote na
mafanikio? Jibu ni “NDIO” yana mahusiano makubwa sana kuliko unavyofikiri,
kwani maamuzi ndio yanayomfanya mtu afikie hitimisho flani ambalo laweza kuwa
zuri au baya.
Lakini maamuzi haya yanaweza kuwa na hitimisho baya pale mtu
anapohitimisha maamuzi hayo vibaya, mfano mtu ambae kakutana na maisha
magumu na akaamua kujinyonga kutokana na ugumu wa maisha hayo mtu huyu ameamua kuchukua maamuzi mabaya
ambayo suluhisho lake si kujinyonga bali lilikuwa ni kupambana na maisha hayo
mpaka kuhakikisha anafanikiwa.
Hata wewe unapaswakuwa na maamuzi magumu lakini yenye matokeo chanya
katika maisha yako ili kuhakikisha unafikia malengo yako bila kuangalia wengine
watakuonaje au watakuchukuliaje juu ya maamuzi unayotaka kuyachukua chamsingi
maamuzi hayo baada ya kuyafanya yawe na matokeo chanya.
Kwahio ili ufanikiwe unahitaji kuwa na maamuzi magumu ambayo muda
mwingine unaweza kujikuta hakuna anaekuunga mkono juu ya maamuzi hayo au
unaweza kujikuta unasemwa sana na watu juu ya maamuzi hayo wewe usitikiswe na
maneno ya watu simamia hicho ulichokiamua ilimradi tu kiwe na matokeo chanya
ambayo yatakuja kuwa ni mafundisho tosha kwa wale waliokuona kuwa umekosea kufanya
maamuzi kwa wakati ule.
Unaweza kujiuliza kuwa ni maamuzi gani magumu ambayo napaswa
kuyachukua ili nifanikiwe? Ni haya hapa maamuzi magumu ambayo unapaswa
uyachukue ili ufanikiwe ;
1. 1. Kuachana na marafiki wasio na
mchango wowote katika maisha yako.
Ili ufanikiwe unahitaji kuzungukwa na marafiki ambao mawazo yao
yanawaza kufanikiwa tu, ukijikuta una marafiki wengi ambao wanawaza kula,
kulala, kuamka, kucheza magem, kucheza michezo ya betting, kuchati whatsap,
facebook,au marafiki wanaowaza wasichana kila wakati, maafiki wanaotukana
matusi tukia wakati jua kwamba hata wewe
utakuwa kama wao na ukweli ni kwamba kamwe hutoweza kufikia malengo yako hata
sikumoja.
Jambo la msingi ili wewe kufikia katika malengo yako chukua uamuzi
mgumu wa kuvunja urafiki na watu kama hao kwani ukiendelea kuwa nao wanakuandaa
kuwa tajiri wa umasikini milele katiaka maisha yako. Najia ni ngumu kuachana na
watu uliowazoea lakini hunabudi kuachana nao ili kufikia njozi zako. Na
utakapoachana nao tarajia kuchukiwa, kusemwa, kutukanwa na kufanyiwa mambo
mengi ila hayo yasikukatishe tamaa wewe ziba masikio na fumba macho yako lenga
(focus) kwenye malengo uliojiwekea uatafanikiwa.
2. 2. Kuachana na vitu unavyopenda
kuvifanya sana na vinavyotumia muda bila faida.
Nimuhimu kuchukua maamuzi magumu juu ya vitu uvipendavyo kuvifanya
lakini visivyokuletea faida katiaka maisha yako, najua nivigumu kuachana na
vitu hivyo lakini jua kwamba ndivyo vinavyokufanya usiwe na maisha mazuri
ambayo unayahitaji hivyo ili uwe na maisha mazuri maisha ambayo unajua
yatakuawa na fraha unapaswa kuachana navyo.
vitu hivyo ni kama vile
utumiaji wa mitandao ya kijamii katika shughuli ambazo hazina faida mfano mtu
anakaa asubuhi mpaka jioni yuko online whatsap, facebook, twitter, instagram anachati
tu au anakazi ya kupost picha kialsiku na kutafuata like nyingi napenda
nikwambie kuwa huo muda unaoutumia katika shughuli hizo za kuchati ni mwingi
sana na kama ungelibuni kitu chakufanya ungelifika mbali sana.
Kumbuka kuwa walioanzisha mitandao hio wao wanaingiza kipato kikubwa
sana hivyo nakusihi rafiki achana na kupoteza muda kuchati katikamitandao ya
kijamii bila faida bali tumia mitandao hio katika kujifunza vitu kutangaza
biashara zako na kufanya mambo mengine ambayo yatakuletea faida katika maishha
yako na si vinginevyo hapo ndipo utafanikiwa, najua ni vigumu kwakuwa
ushaathiriwa na mitandao hio lakini unapaswa uchuke uamuzi mgumu ili kuokoa
maisha yako kwani uko hatarini.
3. 3 . Heshimu ratiba yako.
Ili ufanikiwe unahitaji kuheshimu ratiba uliojiwekea lasivyo
utajikuta unapoteza muelekeo wa unakoelekea. Unapaswa usimamie ratiba yako
wakati wote na usikubali mtu akavuruga ratiba hio kwan atakuwa ameharibu
uelekeo wako wote.
Wapo watu ambao wanaweka ratiba zao lakini wanakuja kuvurugiwa
ratiba zao kwasababu tu hawana maamuzi juu ya kile walichojiwekea, utakuta mtu
labda saa mbili ni mda wakusoma anajikuta anashawishiwa na rafikiyake kwenda
kutembea nae anaenda bila kutambua kuwa anavuruga ratiba yake.
Rafiki bora watu wakuone unaringa kuliko kuharibu ratiba yako ili
kuwafurahisha nafsi zao kwa vitu visivyokuwa katika ratiba yako kwa siku hio,
kama mtu akija anahitaji mkatembee au anahitaji mpige stori na ukiangalia ni
muda wako wakusoma mwambie haiwezekani kwakuwa muda huu ni muda wa kusoma
usimfiche unapaswa umwambie hata kama atakuona unaringa ni sawa lakini atakuwa
amejifunza kitu kutoka kwako kuwa muda flani unafanya kitu flani na muda flani unafanya
kituflani kwahio si rahisi mtu kukuhamisha katika malengo yako chamsingi kuwa
na maamuzi magumu juu ya ratiba yako usiwe kama bendera inayofwata upepo.
Mwisho mapenda nikwambie kuwa” UNAHITAJI MAAMUZI MAGUMU ILI KUFIKIA
MALENGO YAKO”
Ahsante kwa kutumia mudawako katika kusoma makala hii siku ya leo
naamini umejifunza vitu siku ya leo hivyo kwakuwa wewe umejifunza vitu usisahau
kushea ujumbe huu ili na wengine wapate kujifunza ulichojifunza wewe.
Pia napenda kukualika kuwa kama hujajiunga na ukurasa wangu wa “ONA
MBALI” ulioko facebook muda ndo huu jiunge sasa kwani katika ukurasa huu utajifunza
mengi sana ambayo naamini yatabadili maisha yako.
Ili kujiunga na ukurasa huu
uliopo facebook sachi neno “ONA MBALI” kisha bonyeza neno “FOLLOW” alafu pia
bonyeza neno “ LIKE” nawe utakuwa
umejiunga na ukurasa huu wa “ONA MBALI”
Pia karibu katika blog yangu kupitia
www.onambali.blogspot.com
kwa makala nyingi zaidi.
Ila kwa ushauri zaidi au maoni yoyote waweza wasiliana nami kupitia;
Emai: daude950@gmail.com
Sim: 0679329339
EMMANUEL DAUD
BLOGGER WAKO APENDAE UFANIKIWE
I like it thax
ReplyDeleteNi kweli kabisa
ReplyDelete